Posted On December 20, 2024

Tanzania Mpya, Dira Mpya: Toa Maoni Yako Kwenye Dira ya Maendeleo 2050!

AGCOT 0 comments

Wadau wa SAGCOT, wanufaika, na washirika wote, mnakaribishwa kushiriki katika kongamano muhimu la mtandaoni kujadili Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.


📅 Tarehe: Jumatatu, 23 Desemba 2024
Muda: Saa 4:00 asubuhi – 6:00 mchana
📍 Mahali: Mtandaoni kupitia Microsoft Teams


Rasimu ya Dira ya Maendeleo 2050

Rasimu hii, iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, inalenga kuweka msingi wa maendeleo endelevu ya Tanzania kuelekea mwaka 2050.

Kwa sasa, Dira imeingia katika awamu ya uhakiki, ambapo maoni ya wadau kutoka sekta mbalimbali ni muhimu kuhakikisha inaakisi mahitaji na ndoto za Watanzania wote.

Hatua Zinazofuata

🔹 Ushirikishwaji wa Wadau: Desemba 2024 – Januari 2025
Kama alivyoeleza Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji,, kipindi hiki ni fursa ya pekee kwa wadau kutoa maoni yao na kushiriki katika kujenga Tanzania mpya.


Kwa Nini Kushiriki ni Muhimu?

Huu ni wakati wako wa:

  • Kuchangia maoni katika mustakabali wa kilimo, uchumi, na maendeleo ya kijamii.
  • Kuimarisha ushirikiano kati ya wadau wa kilimo na maendeleo ya kitaifa.
  • Kusaidia kuhakikisha Dira hii inaleta matokeo chanya kwa kila Mtanzania.

👉 Jiunge Sasa: Bonyeza Hapa
Au tumia QR Code iliyopo kwenye bango la tangazo.


Usikose! Toa Maoni Yako Leo. Pamoja Tunaweza Kujenga Tanzania Mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Post

Demonstrating Agronomic Practices to Increase Soybean Yields in Tanzania – TSSI 2024 Field Results

Tanzania Sustainable Soybean Initiative (TSSI)Report: “Demonstrating Agronomic Practices to Farmers to Increase Soybean Yield –…

Zanzibar: Establishing a Multi-Stakeholder Platform for Sustainable Landscape Management

Zanzibar:The Revolutionary Government of Zanzibar, through the Ministry of Agriculture, Irrigation, and Natural Resources, in…

Boosting Tanzania’s Horticulture Sector: Stakeholders Address Agro-Logistics Challenges

📍 Sunset Hotel, Iringa – 14th March 2025 In a concerted effort to transform Tanzania’s…
Share via
Copy link